• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Tarime Town Council
Tarime Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mtaa Halmashauri ya Mji wa Tarime

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Chimbuko / Asili
      • Ukubwa wa Eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
      • Orodha ya Viongozi
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Raslimali Watu
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Usimamamizi wa Taka na Usafi na Mazingira
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Kitengo cha Michezo Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Kuonana na mwenyekiti
    • Kata
      • Kata ya Bomani
      • Kata ya Kenyamanyori
      • Ketare
      • Nkende
      • Nyamisangura
      • Nyandoto
      • Sabasaba
      • Turwa
    • Wajumbe wa Kamati
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Repoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha

WANANCHI WAHIMIZWA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 TARIME MJI

Posted on: September 26th, 2024

Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Mji Tarime Bi Gimbana E Ntavyo amewaomba viongozi mbalimbali na asasi za kiraia kuwahimiza wananchi kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwakugombea nafasi mbalimba, kujitokeza kujiandikisha na kuwapigia kura viongozi bora

Hayo ameyasema leo kwenye ukumbi wa wa Halmashauri ya Mji wakati akitoa maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024 katika Halmashauri ya Mji huku akisisitiza elimu ya mpiga kura ikitolewa kwa ufasaha wananchi watajitokeza wengi

"Sisi kwa umoja wetu kwenye maeneo yetu tukitoa elimu hii vizuri kwa wananchi naamini kabisa watajitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwani ni haki yao kikatiba kuanzia kugombea nafasi, kujiandikisha kwenye daftari kwa mtaa husika na kupiga kura siku ya tarehe 27, Novemba mwaka huu" amesema Gimbana

Aidha, amewataka viongozi hao pia wawashauri wanawake wenye sifa za kugombea katika jamiii kuja kuchukua fomu ili kuwania nafasi mbalimbali za Serikali za mitaa katika Halmashauri hiyo

"Zoezi la ugawaji fomu ni kuanzia tarehe 1 Novemba 2024 hadi tarehe 7 Novemba 2024 kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa kumi kamili jioni Hivyo washaurini wanawake wenye sifa za kugombea kwenda kuchukua fomu pia za kugombea" amesema Gimbana

Uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika tarehe 27, Novemba 2024, huku zoezi la wananchi kujiandika katika daftari la wapiga kura litaanza tarehe 11 hadi tarehe 20, Octoba 2024 katika mitaa yote 81 kutakuwa na vituo kuanzia majira ya saa 2 kamili asubuhi na kufungwa saa 12 kamili jioni kauli mbiu ni " Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, jitokeze kushiriki Uchaguzi"


Matangazo

  • TANGAZO LA UPANGISHAJI WA MAENEO YA BIASHARA KATIKA SOKO KUU LA HALMASHAURI YA MJI TARIME May 23, 2025
  • Angalia yote

Habari Mpya

  • MADIWANI TARIME MJI WAMONGEZA RAIS SAMIA

    May 30, 2025
  • SOYA ONE LIMITED YACHANGIA GUNIA 20 ZA MAHINDI KWA SHULE ZA MSINGI TARIME MJI

    May 20, 2025
  • WANANCHI WAJITOKEZA KWA WINGI MAFUNZO YA UOMBAJI WA VIBADANDA SOKO KUU TARIME

    May 15, 2025
  • MADIWANI WARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA MIRADI MBALIMBALI TARIME MJI

    May 15, 2025
  • Angalia yote

Picha ya Mwendo

DAS TARIME AITAKA TARIME TC KUSIMAMIA USAFI
Picha za video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Takwimu za Haraka
  • Hati ya Mshahara (Watumishi Portal)

Viunganishi Linganifu

  • OR- TAMISEMI
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
  • Wizara ya Nishati na Madini.
  • Tovuti ya Mkoa wa Mara
  • Tovuti Rasmi ya Rais

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HRO JOSEPH HAYMO

    Anuani ya Posta: 45, Tarime

    Simu: 0784635368

    Simu ya Mkononi: 0784635368

    Barua Pepe: utawala@tarimetc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©Tarime Town Council . All rights reserved.