• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Tarime Town Council
Tarime Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mtaa Halmashauri ya Mji wa Tarime

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Chimbuko / Asili
      • Ukubwa wa Eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
      • Orodha ya Viongozi
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Raslimali Watu
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Usimamamizi wa Taka na Usafi na Mazingira
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Kitengo cha Michezo Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Kuonana na mwenyekiti
    • Kata
      • Kata ya Bomani
      • Kata ya Kenyamanyori
      • Ketare
      • Nkende
      • Nyamisangura
      • Nyandoto
      • Sabasaba
      • Turwa
    • Wajumbe wa Kamati
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Repoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha

WAGANGA WAKUU TANZANIA WAMEMTUNUKIA RAIS SAMIA TUZO

Posted on: July 12th, 2025

*Waganga Wakuu wamemtunukia Rais Tuzo, Mhe. Mpango 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa tuzo maalum ya kutambua mchango wake kwenye Sekta ya Afya na Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri hii leo.

Tuzo hiyo ameitoa  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya Waganga hao na kumkabidhi Makamo wa Rais, Mhe. Dkt. Philipo Mpango aliyekuwa mgeni rasmi katika Mkutano huo wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri jijini Dodoma.

Mbali na tuzo hiyo pia Waganga Wakuu wamemtunukia Makamo wa Rais tuzo hiyo pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe Mohamed Mchengerwa na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama.

Mhe. Mpango  amewapongeza Waganga Wakuu nchini

kwa kazi wanayofanya ya kuwahudumia  wananchi huku akiwataka waendelee

kuimarisha huduma na sekta ya afya kwa ujumla na kuzingatia maadili ya taaluma yao.

Amesisitiza kuwa Serikali itatekeleza mara moja maombi ya kuboresha stahili za wataalam hao kulingana hali halisi ya uchumi.

"Nawaelekeza Mawaziri wa Afya na OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na Waziri wa Fedha washughulikie suala la ucheleweshaji wa posho za madaktari na wahudumu wa afya." Amesisitiza Mhe. Mpango

Amesema kwa sasa Serikali inapoelekea kutekeleza mpango wa Bima ya Afya kwa Wote Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatakiwa  kuhakikisha zinasimamia vema ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha yanatumika kiadilifu ili kuboresha zaidi utoaji wa huduma.

Pia amewapongeza Wakuu wa Mikoa na Wilaya, pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri/Manispaa na Majiji kwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwemo ile ya afya na vifaa tiba katika Halmashauri/Manispaa/Majiji.

Amesema ili kuimarisha huduma za afya na usimamizi shirikishi, Serikali imenunua na kusambaza magari ya kubeba wagonjwa (ambulance) na  mashine za kisasa za kidijiti (Digital X-ray na ultrasound) na kuagiza kuvitunza vifaa hivyo na vingine vitakavyonunuliwa ili viweze kutumika kwa muda mrefu na kutoa huduma kwa watu wengi zaidi.

Akimkaribisha Mhe. Mpango kutoa hotuba, Mhe.Mchengerwa amemshukuru Rais Samia kwa maono yake makubwa na miongozo kwenye sekta ya afya ambayo yameleta mapinduzi makubwa katika kipindi kifupi.

Mhe. Mchengerwa ametumia mkutano huo kutaja mafanikio lukuki yaliyopatikana katika kipindi hiki.

Aidha, amesema  mafanikio hayo pia yanatokana na ushirikiano baina ya Wizara yake na Wizara ya Afya.

Katika mkutano huo wadau mbalimbali ya afya pia wametunukiwa vyeti vya kutambua michango yao.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU 2025 NGAZI YA MKOA NA WILAYA July 05, 2025
  • TANGAZO LA UPANGISHAJI WA MAENEO YA BIASHARA KATIKA SOKO KUU LA HALMASHAURI YA MJI TARIME May 23, 2025
  • Angalia yote

Habari Mpya

  • MWENGE WA UHURU WAZINDUA,WATEMBELEA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI MIRADI YA 1.8 BILIONI TARIME MJI

    August 22, 2025
  • RC MTAMBI AWAONGOZA VIONGOZI NA WANANCHI KILELE CHA NANENANE NYAKABINDI

    August 08, 2025
  • MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI NGAZA KATA TARIME MJI YAHITIMISHWA

    August 06, 2025
  • WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI WALA KIAPO NA KUANZA MAFUNZO TARIME MJINI

    August 04, 2025
  • Angalia yote

Picha ya Mwendo

HOTUBA YA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO LA TARIME MJINI
Picha za video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Takwimu za Haraka
  • Hati ya Mshahara (Watumishi Portal)

Viunganishi Linganifu

  • OR- TAMISEMI
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
  • Wizara ya Nishati na Madini.
  • Tovuti ya Mkoa wa Mara
  • Tovuti Rasmi ya Rais

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HRO JOSEPH HAYMO

    Anuani ya Posta: 45, Tarime

    Simu: 0784635368

    Simu ya Mkononi: 0784635368

    Barua Pepe: utawala@tarimetc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©Tarime Town Council . All rights reserved.