• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Tarime Town Council
Tarime Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mtaa Halmashauri ya Mji wa Tarime

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Chimbuko / Asili
      • Ukubwa wa Eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
      • Orodha ya Viongozi
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara/Vitengo
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Maji
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Sekondari
      • Idara ya Afya
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango na Takwimu
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Ugavi na Manunuzi
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • TEHAMA
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Kuonana na mwenyekiti
    • Kata
      • Kata ya Bomani
      • Kata ya Kenyamanyori
      • Ketare
      • Nkende
      • Nyamisangura
      • Nyandoto
      • Sabasaba
      • Turwa
    • Wajumbe wa Kamati
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Repoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha

Kamati ya Siasa ya Wilaya CCM yafanya ziara kuangalia utekelezaji wa Ilani ya CCM

Posted on: September 26th, 2018

Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi imefanya ziara kutembelea miradi katika Halmashauri ya Mji wa Tarime kukagua utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi kwa robo kwanza mwaka wa fedha 2018/2019. "Chama tawala ndio chenye wajibu wa kuisimamia Serikali, utekelezaji wa Irani ya CCM katika Wilaya ya Tarime ni lazima usimamiwe kwa karibu na Chama chenye Serikali ili kuhakikisha wananchi wanatatuliwa shida zao" Maneo hayo yalisemwa na Katibu wa CCM wa Wilaya Ndugu Hamisi Mkaruka Kura.

Miradi iliyokaguliwa na Kamati ya siasa ni Miradi sita:

1: Kuangalia Hati iliyolejeshwa kwa Halmashauri baada ya Kufutwa na Mhe Rais.

Hati ya Shamba Namba Tatu la Nyandoto lililokuwa likimilikiwa na Ndg Magrya Mwita Chacha lililejeshwa katika Halmashauri ya Mji wa Tarime. Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi iliweza kujionea hati hiyo na kupata maelezo ya kina kutoka kwa Kaimu Afisa Ardhi kuwa bado kuna maeneo mengine ya ardhi yanayomilikiwa isivyo halali yanafuatiliwa ili hati zake zilejee Halmashauri. Kamati ya siasa imepongeza juhudi hizi za watendaji ambazo zitawafanya wanachi wengi wa Tarime wapate maeneo kwa ajili ya makazi.

Kamati ya siasa ikiwa katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Wakiangalia Moja ya hati ya shamba lililokuwa likimilikiwa na Mmiliki Magrya Mwita Chacha.

2: Mradi wa Kisima cha Maji cha Magena.

Kamati ya siasa ilitembelea Mradi wa Maji ulioko Magena kata ya Nkende.


Mradi huu wa Maji umekamilika na uhadumia wa Kijiji cha Magena na sehemu za jirani, mradi unasimamiwa na Kamati ya Maji ya Kijiji. Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi imelidhishwa na utekelezaji wa Mradi huu ambao utawafanya wananchi wa maeneo hayo kupata nafuu kubwa ya kufuata maji mbali.

3: Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Magena.

Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi ilikwenda kuangalia mradi wa Kituo cha Afya unaojengwa Magena. Katibu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Hamisi Mkaruka alipewa taarifa fupi ya mradi huo kutoka kwa Eng Tungu kuwa Serikali ya chama cha Mapinduzi imeishatoa kiasi cha shilingi za kitanzania Milioni 400 ambazo ni za awamu ya kwanza.

Diwani wa kata ya Nkende, Mhe Komotte amesema kuwa wananchi wa Magena wameanza kuchangia katika kutoa Ardhi yenye thamani ya shilingi Milioni 10, wananchi wamechangia nguvu zao katika uchimbaji wa msingi, Tripu 25 za mawe zenye thamani ya shilingi milioni mbili na laki tano zimetolewa na wananchi, Mchanga wa thamani wa shilingi milioni mbili na laki mbili sawa na tripu 22 zimeishaitalewa na wananchi, vilevile Kila kaya imetoa kiasi cha shilingi 5,000. Mhe Diwani Komote amesema bado wananchi wanaendelea kuchangia nguvu zao pamoja na vifaa vya ujenzi ili kuhakikisha Kituo hicho cha Afya kinamalizika mapema na kuanza kazi.

4: Mradi wa Ufugaji Nyuki.

Kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi imetembelea na kuangalia utekelezaji wa Ilani ya CCM. Kamati ilifika katika Kata ya Nkende na kuangalia mradi wa ufugaji nyuki unaofadhiliwa na Halmashauri na wanakikundi wenyewe. Kikundi cha Romoli kilipewa Jumla ya Tsh 405,000/= na kikundi chenyewe kimetoa kiasi cha shilingi 456,000 hivyo kufanya jumla ya Tsh 861,000/= ambazo zilitumika katika kutengenezea Mizinga ya nyuki na usimikaji wa Mizinga hiyo. Kikundi cha Romoli kina jumla ya wanachama 35 na kikiwa na jumla ya mizinga 43. Kamati ya siasa imepongeza mradi huu kwani imekuwa ni sehemu ya ajira kwa wanachama wake na imesaidia katika utunzaji wa Mazingira.


5: Mradi wa Madarasa Mawili katika Shule ya Sekondari Mogabiri.

Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi imekaguwa na kuangalia utekelezaji wa Ilani ya chama cha mapinduzi kwenye upande wa Elimu. Shule ya Sekondari Mogabiri inatekeleza wa Mradi wa Ujenzi wa Madarasa mawili. Kamati ya siasa imelidhishwa na hatua ya mradi huo.

6: Utunzaji wa Mazingira katika Chanzo cha Maji Nyandurumo:

Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi imetembelea na kuangali utunzwaji wa Mazingira katika Chanzo pekee cha Maji katika Mji wa Tarime. Kaimu Afisa Mazingira aliieleza Kamati ya Siasa kuwa miti yote ambayo si rafiki kwa chanzo hicho tayari imekatwa na wananchi wanaozunguka chanzo cha Nyandurumo wamepewa Elimu ya kutosha kuhusu utunzaji wa Mazingira kuzunguka chanzo hicho. Hata hivyo Katibu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Hamisi Mkaruka ameitaka Halmashauri kuchimbua visiki vya miti visivyo rafiki na chanzo cha maji ili isichipue na kupandwa miti rafiki katika chanzo hicho cha Maji. Kamati ya siasa imeridhishwa na hatua zinazochukuliwa na watendaji wa Halmashauri katika kuhakikisha chanzo hicho kinadumu kwa muda mrefu.


7: Zahanati ya Gamasara, Mradi wa CHF na ICHF

Kamati ya siasa imepita katika Zahanati ya Gamasara kuangalia mradi wa CHF na ICHF iliyoboreshwa. Kamati imepewa taarifa kuwa mwamko wa wananchi katika kupata huduma kupitia Bima (ICHF) ni mkubwa, "wananchi wana mwamko mkubwa katika kupata huduma kupitia bima hii" alisema Rahabu Mfungo Mkuu wa Zahanati hiyo. Kamati ya siasa imeshauri kuwa juhudi za kusajili wananchama katika bima mpya iliyoboreshwa ili wananchi wapate huduma hata wakati hawana pesa.



8: Kikundi cha Wanawake Walemavu:

Katika utekelezaji wa Ilani ya CCM, Halmashauri ilitoa mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali vipatavyo nane. Kikundi cha wamama walemavu ni moja ya vikundi vilivyonufaika na mikopo. Katibu wa kikundi hicho Bi Rozilina Masiroli ameiambia kamati ya siasa kuwa walianza na cherehani mbili lakini mpaka sasa wanazo cherehani kumi kikundi kimesajiliwa na wana akaunti banki ambayo iko hai na wameisha shiriki kwenye maonesho mbalimbali katika sehemu tofauti tofauti nchini Tanzania.


WAJUMBE WA KAMATI YA SIASA NA SEKRETARIETI YA CCM WILAYA YA TARIME WALIOSHIRIKI ZIARA YA KUANGALIA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM.

1: HAMIS MKARUKA KURA - KATIBU WA CCM (W)

2: MAREMA SOLLO - KATIBU WA SIAASA NA UENEZI (W)

3: NURU HOTAE  - MJUMBE WA KAMATI YA SIASA (W)

4: TIBOCHE RICHARD - MJUMBE KAMATI YA SIASA (W)

5: SAMWEL MANGARAYA - MJUMBE KAMATI YA SIASA (W)

6: JOYCE WILLIAM - MJUMBE KAMATI YA SIASA (W)

7: GODIFRAY FRANCIS - MJUMBE KAMATI YA SIASA (W)

8: MATHIAS LUGOLA - MJUMBE KAMATI YA SIASA (W)

9: NEWTON MUONG -  MJUMBE KAMATI YA SIASA

10: SAUDA H. KASHOMBO - MJUMBE KAMATI YA SIASA

Matangazo

  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI HALMASHAURI YA TARIME MJI December 16, 2020
  • Tangazo la Zabuni ya Upimaji wa Viwanja Katika Mji wa Tarime February 20, 2019
  • Tangazo la Kazi Mhandisi Mshauri na Msimamizi Mradi wa Soko la Kisasa February 20, 2019
  • TANGAZO LA UKODISHAJI WA JENGO LA MAMLAKA YA MAJI, HALMASHAURI YA MJI WA TARIME November 10, 2017
  • Angalia yote

Habari Mpya

  • MATOKEO DARASA LA NNE, KIDATO CHA PILI NA KIDATO CHA NNE

    January 15, 2021
  • Kikao Cha Elimu ya Afya PHC

    August 29, 2019
  • Kamati ya Siasa ya Wilaya CCM yafanya ziara kuangalia utekelezaji wa Ilani ya CCM

    September 26, 2018
  • Pikipiki Mpya kwa Maafisa Elimu Kata

    September 25, 2018
  • Angalia yote

Picha ya Mwendo

Siku ya Mazingira Duniani Kufanya Butiama Kitaifa
Picha za video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Takwimu za Haraka
  • Hati ya Mshahara (Watumishi Portal)

Viunganishi Linganifu

  • OR- TAMISEMI
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
  • Wizara ya Nishati na Madini.
  • Tovuti ya Mkoa wa Mara
  • Tovuti Rasmi ya Rais

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©Tarime Town Council . All rights reserved.